NA DIRAMAKINI
WANAFUNZI 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na vyuo vya fani mbalimbali.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 yanaonesha kuwa, watahiniwa 192,348 walipata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kati yao Tanzania Bara walikuwa watahiniwa 188,128 wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.
Akizungumza na waandishi wa habari , leo Jumapili Juni 11, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angelah Kairuki amesema zoezi hilo limezingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 kutoka Tanzania Bara.
Amesema, wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka katika shule za serikali, binafsi, watahiniwa wa kujitegemea, waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.
OFISI YA RAIS - TAMISEMI
UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2023
BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGWA KWENDA SHULE MOJA
CHAGUA MKOA ULIKOSOMA
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |