NA GODFREY NNKO
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa,licha ya ukwasi wa dola kuathirika duniani kutokana na hatua iliyochukuliwa na Marekani kuongeza riba katika soko lake, hapa nchini hali ni himilivu.
Hayo yamebainishwa leo Juni 6, 2023 na Mkurugenzi wa Tafiti na Sera za Uchumi wa BoT, Dkt.Suleiman Missango katika ofisi ndogo za makao makuu BoT jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba wakati wa semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa uchumi Tanzania.
"Kuna upungufu wa fedha,lakini bado sisi kama nchi ni himilivu,kuwa himilivu ina maana bado tunamudu, ukilinganisha na nchi nyingine bado sisi (Tanzania) hali yetu licha ya wote kupigiga na athari zilizotokana na uchumi wa Dunia, lakini sisi hali yetu ni nzuri ukilinganisha na nchi nyingine ambazo tunafanana fanana nazo.
"Kwa nini tunasema bado ni himilivu, kwa sababu bado Benki Kuu inayo akiba ya fedha za kigeni, sasa unaweza kujiuliza kama kuna upungufu, sasa hiyo akiba kwa nini usiimwage tu kule, sasa wewe ukiwa nyumbani kwako unaona bado kuna athari bado zipo,hivi utasema tu kwamba hebu leo ngoja nitumie tu zote? Nafikiri busara ni kwamba hauwezi kutumia zote.
"Na tukasema, baada ya kuona ni himilivu na tunayo akiba ya kutosha,tukasema hii akiba inapaswa kutumika kwa uangalifu, kwa nini kwa uangalifu? Kwa sababu,zile athari bado zipo,hivi vita kati ya Ukraine na Urusi vimeisha?.
"Kwa sababu hatujui vita vitafikia hitimisho lini, inabidi utumie akiba yako kwa uangalifu, hata kama ni nyumbani kwako, unaona kabisa kwamba hivi kwa mfano tulikuwa tunakabiliana na ukame hapa, hivi akiba yako kweli kwa sababu tuna upungufu kidogo, mshahara haujaongezeka au hauna kazi unatumia tu bila utaratibu?. Hapana, ingawa haupo kwenye upungufu.
"Sisi hatupo katika crisis, tuna upugufu. Na kutokana na uhimilivu huo ndiyo maana sisi (Benki Kuu) kila siku tunauza dola milioni mbili kwa mabenki ili yasaidie kile ambacho kipo kule, upungufu si kwamba zimeisha, unaposema kwamba kuna upungufu wa dola huko sokoni inaweza kuwa sahihi, lakini usije ukaaminisha mtu kwamba hazipo, upungufu si kwamba hazipo,na tunauza kila siku iendayo kwa Mungu dola milioni mbili,ndiyo kitu cha kusema tunazitumia kwa uangalifu tunaangalia hali inakwendaje.
"Ndiyo maana jeshini unafundishwa wakati wa vita si tu kwamba unatumia tu silaha zako zote hivi, kwa sababu haujui adui yako, unatumia tu kidogo, unaaza kidogo kidogo hivi, tunaanza na wale wadogo wadogo wa kujitolea kwanza,hauwezi kuanza na majenerali."
Aidha, amefafanua kuwa,kabla ya vita ya Ukraine na Urusi walikuwa hawauzi kabisa dola,badala yake wao ndiyo walikuwa wananunua na kuweka akiba,lakini kadri siku zilivyoendelea wakaanza kuuza kidogo kidogo hadi kufikia kiwango hicho cha dola milioni mbili kwa siku.
Dkt.Missango amefafanua kuwa,hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Marekani kuongeza riba katika soko lake imeathiri mzunguko wa fedha duniani hususani dola ya Marekani (USD), hivyo kuathiri ukwasi wa fedha hiyo muhimu kwa
"Kwa upande wa Marekani, ambao ndiyo huwa wanachapisha dola na ndiyo currency yao, hasa ndiyo wamechukua hatua zaidi ukilinganisha na nchi nyingine duniani.
"Wamepandisha riba kutoka asilimia 0.75 hadi asilimia 5.25 sawa na ongezeko la asilimia zaidi ya 500, maana yake ni kwamba hiyo riba ni kubwa na inavuta dola nyingine zote duniani, kwa sababu ukilinganisha riba hiyo ya Marekani hii ya asilimia 5.25 ndiyo riba zetu, kwa hiyo kila mmoja sasa mwenye dola anapeleka Marekani, kwa hiyo imekausha ukwasi wa dola.
"Kwa hiyo hii ni sababu moja wapo, ya mwenendo wa dunia kuleta matatizo." Amesema, pia ongezeko la namna hiyo huwa linaathiri mataifa kukopa,kutokana na ongezeko kubwa la riba."
Amesema, Serikali ya Marekani ilichukua hatua hiyo ili kuvutia wawekezaji sambamba na kuimarisha soko lake kutokana na kuongezeka mfumuko wa bei uliosababishwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi.
Miongoni mwa changamoto hizo, Dkt.Missango amebainisha ni pamoja na UVIKO-19,vita kati ya Urusi na Ukraine ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi.
“Kutokana na changamoto ya Uviko-19,mabadiliko ya tabia nchi na vita ya Ukraine na Urusi katika uchumi wa Dunia, benki ziliamua kubadilisha mwelekeo wa sera ya fedha kwa kupandisha riba.Baada ya kuyumba kwa uchumi, Marekani iliamua kuongeza kiwango cha riba kwenye soko lake.
“Ongezeko hilo limechochea uwekezaji katika soko lake na kusababisha upungufu katika soko la nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania,”amesema Dkt.Missango.
Pia ameeleza, kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa, mwenendo wa uchumi wa Dunia sio wa kuridhisha kutokana na changamoto hizo tatu. Huku akibainisha kuwa, Urusi na Ukraine wana mchango mkubwa katika uchumi wa Dunia hususani upande wa uzalishaji wa chakula, mafuta na gesi yakiwemo makaa ya mawe.
“Urusi na Ukraine wanazalisha robo tatu ya ngano inayozalishwa duniani. Urusi ni ya pili kwa kuzalisha gesi asilia duniani, pia ni ya tatu katika uzalishaji mafuta na inazalisha asilimia sita ya makaa ya mawe duniani.
“Aidha,Ukraine inazalisha kiwango kikubwa cha mafuta ya kula na mahindi. Unaweza kuona ni kwa namna gani vita hiyo imechangia tatizo la uchumi duniani,”amesema Dkt.Missango.
Wakati huo huo, Dkt.Missango amesema,dola za Marekani zinatarajiwa kuongezeka katika kipindi cha Julai na Septemba, mwaka huu kutokana na matarajio ya ongezeko la watalii hapa nchini.
Fedha za kigeni
Hivi karibuni, Benki Kuu ya Tanzania imetoa maelekezo kwa taasisi za fedha zinazojihusisha na biashara ya fedha za kigeni namna ya kuendesha biashara hiyo kwa lengo la kulinda utulivu wa uchumi mpana na uthabiti wa mfumo wa kifedha nchini.
Katika maelekezo hayo mapya, miamala yote ya fedha za kigeni inayozidi thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1.0 kwa muamala mmoja katika soko la rejareja, lazima ifanyike kwa bei ya soko la fedha za kigeni baina ya benki.
Aidha, miamala yote ya mteja mmoja kwa siku itajumlishwa ili kujua jumla ya kiasi husika. Katika sekula yake kwa taasisi hizo zinazojihusisha na biashara ya fedha za kigeni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema ni marufuku kufanya biashara ya fedha za kigeni na madalali wa kimataifa wa fedha za kigeni ambao hawajasajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, madalali na wafanyabiashara wa fedha za kigeni hapa nchini wanatakiwa wakati wote kuzingatia utaratibu wa kumtambua mteja (KYC) kabla ya kufanya naye biashara hiyo.
Katika maelekezo hayo, kiwango cha juu cha mizania kati ya mali na amana katika fedha za kigeni (foreign exchange Net Open Position (NOP)) kitakuwa asilimia 10 ya mtaji wa msingi (core capital) na kinatakiwa kuzingatiwa wakati wote.
Alielekeza pia kwamba Barua za Udhamini (Letters of Credit (LCs)) za shehena zinazopitia hapa nchini (transit cargoes) zitatokana na fedha za kigeni kutoka katika nchi ambako shehena hizo zinakwenda.
“Inasisitizwa kwamba uzingatiaji wa matakwa yaliyoainishwa hapa ni wa lazima na kutakuwa na usimamizi na ukaguzi kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kukiuka maelekezo haya kutasababisha adhabu kama zinavyoelezwa katika Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992,” alieleza Gavana Tutuba.
Utekelezaji wa maelekezo ya uendeshaji wa huduma za fedha za kigeni kulingana na mahitaji ya sasa ya soko ulianza rasmi Juni Mosi, 2023.
Aidha, maelekezo hayo mapya yalifutia maagizo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania tarehe 6 Agosti 2020.“Benki inawakumbusha wahusika wote wa huduma za fedha za kigeni kuzingatia matakwa ya mpango wa fedha za kigeni nchini muda wote,”alielekeza Gavana.