Bunge lapitisha kwa asilimia 100 bajeti ya Trilioni 15.94/- Wizara ya Fedha na Mipango


Awali Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Waziri Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (MB) amesema, katika mwaka 2022/23 aliliomba Bunge ridhaa ya kutumia jumla ya shilingi trilioni 15.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu yake tisa ya kibajeti, ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 15.38 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 564.22 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Aidha, Bunge liliombwa liidhinishe shilingi bilioni 97.13 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 87.72 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 9.41 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news