CCM yaomboleza kifo cha Mohamed Raza Hassanali

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepokea kwa masikitiko na huzuni mkubwa taarifa ya kifo cha Kada,Mwanasiasa na Mfanyabiashara maarufu Ndugu Mohamed Raza Hassanali aliyefariki leo Juni 08,mwaka 2023 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es saalam.
Ndugu Mohamed Raza,amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za ndani ya Chama na Serikali ambazo ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja na Mshauri wa Rais wa Zanzibar awamu ya tano katika masuala ya Michezo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki,Wana CCM na Watanzania wote walioguswa na msiba huo amewasihi waendelee kuwa na subira katika kipindi chote cha msiba huo.

“Enzi za uhai wake Mohamed Raza alikuwa ni kiongozi aliyelinda na kukipigania Chama chetu na alikuwa ni kada muadilifu,mchapakazi na mzalendo mwenye maono ya kimaendeleo ndani ya Chama na Serikalini”, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi.

Ndugu Raza, alizaliwa Julai 08,1962 katika Mtaa wa Mkunazini Unguja, hadi anafariki alikuwa ni Kada wa CCM na Mfanyabiashara anatarajiwa kuzikwa leo saa 11:00 jioni Juni 08,mwaka 2023 katika Makaburi ya Kisutu Dar es saalam.

Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news