DC wa Maswa aunga mkono juhudi za REA kuhamasisha wananchi vijijini kuunganisha umeme

NA VERONICA SIMBA-REA

MKUU wa Wilaya ya Maswa, Mheshimiwa Aswege Kaminyonge amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali katika wilaya hiyo kuunga mkono na kuendeleza jitihada zinazofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) za kuelimisha na kuhamasisha wananchi wa vijijini waliofikiwa na miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa kwa kuunganisha nishati hiyo na kuitumia kujiletea maendeleo.
Alitoa wito huo Juni 28, mwaka huu wakati akizungumza na timu maalumu kutoka REA na TANESCO iliyopo wilayani Maswa mkoani Simiyu kwa kazi ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuunganisha umeme.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mheshimiwa Aswege Kaminyonge akizungumza na Timu maalumu kutoka REA na TANESCO iliyopo wilayani Maswa mkoani Simiyu kwa kazi ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi vijijini kuunganisha umeme. Taswira hii ilichukuliwa Juni 28, 2023.
"Niwaahidi kwamba, mimi na viongozi wenzangu tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono na kuendeleza kazi hii nzuri ya kuwahamasisha wananchi wetu hususani ambao wamekwishafikiwa na miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa hii ili kuboresha zaidi hali zao kiuchumi na hata kijamii."
Msimamizi wa Miradi ya REA, Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mheshimiwa Aswege Kaminyonge (haonekani pichani) kuhusu utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini wilayani humo, Juni 28, 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa REA na timu hiyo ya Uhamasishaji, Msimamizi Miradi wa REA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale alisema, azma ya Serikali siyo tu kuwafikishia nishati bora wananchi wa vijijini bali pia kuhakikisha wanazitumia kwa lengo la kuboresha maisha yao na ya Taifa kwa ujumla.
Pamba ni mojawapo ya zao la kibiashara mkoani Simiyu. Upatikaji wa umeme vijijini mkoani humo umewezesha kujengwa kwa viwanda vidogo vya kuchambua pamba hivyo kuwanufaisha wakulima.
Saluni za kunyoa ni miongoni mwa shughuli za kijasiriamali zinazofanywa na wananchi vijijini ili kuboresha maisha. Upatikanaji wa umeme vijijini umechochea kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa shughuli hizo vijijini kama taswira hii iliyochukuliwa katika kijiji cha Buhangija Wilaya ya Maswa, Juni 28, 2023 inavyoonesha.
Uelimishaji na uhamasishaji wananchi vijijini kuunganisha umeme ukiendelea katika vijiji vya Buhangija na Suluwalu vilivyopo Kata ya Mbaragane Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Juni 28, 2023.
Miundombinu ya umeme katika vijiji vya Buhangija na Suluwalu vilivyopo Kata ya Mbaragane, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Taswira hii ilichukuliwa Juni 28, 2023 wakati wa zoezi la uelimishaji na uhamasishaji wananchi vijijini kuunganisha umeme.
Zoezi la uelimishaji na uhamasishaji wananchi kuchangamkia fursa za umeme vijijini ni zoezi endelevu ambapo mpaka sasa zoezi hilo limekwishatekelezwa mkoani Mwanza na kufuatiwa na Mkoa wa Simiyu ambako zoezi linaendelea. Zoezi hilo litafanyika katika Mikoa yote nchini awamu kwa awamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news