NA DIRAMAKINI
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo anawaalika wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kushiriki katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo yataanza Juni 23 na kilele chake ni Juni 25, 2023.
Amesema, katika maadhimisho hayo ambayo yatafanyika jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mgeni rasmi siku ya kilele atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba.”
"Ni heshima kubwa kuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi katika kilele cha kitaifa cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya tarehe 25 Juni, mkoani Arusha."

Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)