NA DIRAMAKINI
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema CCM Zanzibar kupitia rasimali zake inatarajia kuanza kuwalipa posho kila mwezi Mabalozi kwa ngazi ya shina.
Ameyasema hayo leo Juni 11, 2023 katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM ngazi ya Shina, Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Wakati huo huo,Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, CCM ndiyo chama kinachofaa kuongoza Zanzibar.
Pia amehimiza umoja na mshikamano kwa wanachama wa CCM ili kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 huku akiwataka wana CCM kuvunja makundi, watakaoendeleza kuchukuliwa hatua na kamati za maadili za chama.
Vilevile
ametoa rai kufanyika kwa mafunzo ya itikadi kwa ngazi zote kwa viongozi
wa CCM pamoja na kuhimiza kuendelea kufanyika vikao vya kikatiba katika
kila ngazi.
Aidha, Dkt.Mwinyi atatembelea na kukagua miradi ya CCM mkoani humo ikiwemo eneo la Kituo cha Mafuta Mahonda,Kitega uchumi cha CCM Nungwi, eneo la CCM Afisi kuu Kiwengwa, Shamba la CCM na Afisi kuu Kilombero.