NA GODFREY NNKO
KITUO cha Forodha katika Mpaka wa Horohoro jijini Tanga kimeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) ili kufanikisha operesheni kabambe ya kudhibiti na kutokomeza dawa za kulevya zinazoingizwa na kutolewa nchini.
Hayo yamebainishwa Juni 9, 2023 na Afisa Mfawidhi wa Forodha Kituo cha Horohoro jijini Tanga, Odero Ryoba muda mfupi baada ya kufanya kikao cha pamoja na Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akiendelea na ziara katika Mpaka wa Horohoro ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati hiyo kabambe.
"Kwa leo (Juni 9, 2023) tumetembelewa na Kamishna Mkuu (Jenerali) wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA),katika mambo mengi ambayo tumeongea, jambo kubwa ni ushirikiano ambao tumeongea, tutaanzisha ushirikiano kwa pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini.
"Kwani, sisi ndiyo tuko mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mizigo yote ambayo inaingia nchini tunaifanyia ukaguzi ili kuweza kubaini bidhaa ambazo zinaruhusiwa kuingia kihalali ziingizwe na zile ambazo haziruhusiwi kuingia kihalali zisiruhisiwe kuingia nchini.
"Na kupitia elimu ya leo, pia tumekubaliana kwamba tunaanzisha mashirikiano ya kutoa elimu, tutapita vijijini hasa vile vijiji ambavyo vinapakana na mpaka, ambavyo vipo mpakani kwa ajili ya kutoa elimu na hii elimu itakuwa ni shirikishi kwa kupitia wale viongozi wa Serikali za mitaa ili waweze kutusaidia kuhamasisha na kuelimisha wale wananchi wao wanaowazunguka,"amefafanua Odero Ryoba.
Amefafanua kuwa, lengo la kufanya hivyo ni ili kuweza kudhibiti na kutokomeza dawa za kulevya nchini Tanzania.

"Kiukweli, hizi dawa za kulevya zina madhara makubwa sana katika nchi yetu, hakuna asiyejua yanapoteza nguvu kazi na vile vile yanapoteza rasilimali nyingi za Serikali, tunamuahidi Kamishna Jenerali ushirikiano wa kutosha,sisi taasisi zote za Serikali ambazo zipo mpakani Horohoro kwa ajili ya kudhibiti na kutokomeza kabisa dawa za kulevya hasa katika mkoa wetu wa Tanga.
"Tuna elimu, lakini elimu ambayo wametuongezea ni kwamba, unajua dawa za kulevya kadri muda unavyozidi kwenda kuna dawa za kulevya za aina tofauti tofauti zinazidi kutengenezwa, kwa hiyo elimu ambayo wamekuja kutupatia ni namna ya kuweza kubaini aina mbalimbali za dawa za kulevya.
"Dawa za kulevya ambazo sisi tunapambana nazo kwa wingi katika mpaka wetu wa Horohoro ni dawa aina tatu tu, ikiwemo mirungi, bangi na heroine.
"Mpaka sasa hivi ninavyowaambia, mwaka huu wa fedha uliopita tumeshakamata mirungi kwenye magari zaidi ya matatu na tukaripoti na kukabidhi kitengo cha polisi, kwa hiyo uelewa upo, lakini tunahitaji elimu zaidi kwa sababu kila mara hao wasafirishaji wa dawa za kulevya wanakuja na mbinu mbalimbali za namna wanavyoweza kufanikisha hilo,"amefafanua Afisa huyo.
Awali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imebainisha kuwa imeanza operesheni shirikishi na jumuishi katika mipaka mbalimbali ya nchi ili kuwezesha kudhibiti uingizwaji na utoaji wa dawa za kulevya ndani na nje ya nchi.
Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo aliyasema hayo wakati akiendelea na ziara katika Mpaka wa Horohoro jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati hiyo.
"Tuko hapa Horohoro kwenye mpaka ambao ni mkubwa,na unapitisha bidhaa mbalimbali. Na hii ziara tulianza katika Mpaka wa Namanga tumeenda katika mpaka wa Tarakea, mpaka wa Holili na sasa tupo mpaka wa Horohoro.
"Tuna operesheni mbalimbali tunazoziendesha hapa nchini na katika operesheni zetu tumebaini kwamba dawa za kulevya sasa hivi zinapita katika mipaka na baada ya Serikali kuweka miundombinu mizuri, na ya kisasa katika viwanja vya ndege sasa hivi wale wasafirishaji wa dawa za kulevya hawana tena nafasi ya kusafirisha dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege,"amesisitiza Kamishna Jenerali wa DCEA.
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo ameendelea kufafanua kuwa, "Sasa hivi dawa nyingi zinapitia kwenye mipaka, kwenye nchi kavu, lakini pia baharini.
"Kwa hiyo sasa hivi tunachokifanya tunahakikisha kwamba tunatembelea kwenye mipaka yote ili tuhakikishe kwamba tunajenga mahusiano mazuri, tunajenga ushirikiano na taasisi zote za Serikali zilizoko katika mipaka ili kuhakikisha kwamba tunafanya operesheni ya pamoja kwenye mipaka yote.
"Lengo ni kuhakikisha kwamba tunadhibiti dawa za kulevya kuingia nchini, dawa za kulevya ni uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka ambao unatoka nchi nyingine kwenda nchi nyingine,kwa kushirikiana na taasisi za Serikali zilizoko kwenye mipaka yote ambapo zipo taasisi 17 kwenye kila mpaka, tutahakikisha tunafanya operesheni za kutosha kuhakikisha tunadhibiti dawa za kulevya zisiingie nchini, lakini pia zisitoke nchini kwenda nchi nyingine.
"Lakini, pamoja na kufanya hii operesheni tutatoa elimu pia kwa maafisa wote wa taasisi za Serikali zilizopo mipakani ili waelewe pia aina mbalimbali za dawa za kulevya ambazo zinasafirishwa, lakini pia wajue mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kusafirisha hizo dawa za kulevya, ili tuwe na uelewa wa pamoja na tuweze kufanya operesheni za pamoja.
"Lakini pia pamoja na hiyo elimu, tutatoa pia elimu ya kisheria, baada ya sheria yetu kubadilishwa na kuimarishwa zaidi, ili pia waelewe sheria yetu inasemaje kuhusiana na dawa za kulevya. lakini pamoja na elimu hiyo tutakayoitoa kwa maafisa wetu kwenye mipaka yote tutatoa pia elimu kwa jamii zilizoko mipakani ili watusaidie katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya katika jamii na mipaka,"amefafanua Kamishna Jenerali Lyimo.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)