Global Fund kuendelea kuiunga mkono Tanzania

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko wa Dunia katika kufadhili miradi inayotekelezwa kwenye afua za kupambana na UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya nchini kwa lengo la kuendelea kuwa na huduma bora za afya.
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa inayoratibu na kusimamia fedha kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund) – TNCM Dkt. Rachel Mkunde akizungumza jambo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kitete walipotembelea tarehe 9 Juni, 2023.(Picha na OWM).

Pongezi hizo zimetolewa hii leo Juni 9, 2023 na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Crispin Musiba alipotembela na kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika mkoa wa Tabora ambapo walitembelea Hospitali ya Mkoa huu ya Kitete pamoja na kukagua utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa jengo la maabara katika Hospitali ya Mji Nzega.

Bw. Musiba amesema kuwa, ufadhili wa miradi hiyo umeendelea kuleta tija kwa jamii kwa kuzingatia kuwa huduma zinapatika kwa ubora na kuwa na vifaa vinavyosaidia masuala ya kitabibu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya akiongoza kikao cha pamoja na ugeni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa inayoratibu na kusimamia fedha kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund) kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na mfuko wa Dunia katika mkoa huo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo mratibu wa shughuli hii, hivyo tumeweza kujionea maendeleo ya miradi yote hususan namna vifaa vilivyonunuliwa, upanuzi wa maabara katika viwango vizuri ambapo tunaamini mradi utaendela kulifaa Taifa pamoja na mkoa kuendelea kutatua changamoto chache zilizo ndani ya uwezo wa mkoa,"amesema Musiba.
Mganga Mkuu Tabora, Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akifafanua jambo kwa timu iliyotembelea na kukagua maendeleo ya upanuzi wa maabara katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Nzega ambapo ni moja ya mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Dunia.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa inayoratibu na kusimamia fedha kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund) TNCM Dkt. Rachel Makunde ameseama ziara imeongeza tija na umuhimu wa kujionea namna mradi unavyotekelezwa kwa kuzingatia malengo yanayokusudiwa.
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa inayoratibu na kusimamia fedha kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund) Dkt. Rachel Mkunde akioneshwa dirisha la malipo katika Hospitali ya ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko huo.

“Utekelezaji wa afua zilizochini ya Mfuko wa Dunia, zimeendelea kuzaa matunda kwa kuangalia hii ya ujenzi wa emergency department, pamoja na chumba cha maabara katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kitete pamoja na hii ya Nzega, kazi inaenda vizuri na ujenzi wa maabara hapa Nzega inaridhisha,”amesema.

Aliongezea kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuratibu na kusimamia kwa weledi maeneo yanayotekelezwa miradi hii ili kuendelea kutoa huduma bora za kiafya kwa wananchi wote.
Timu ya ziara iliyotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Dunia pamoja na watumishi wa Mkoa wa Tabora, wakikagua moja ya chumba cha mapumziko katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete wakati wa ziara hiyo. 

Aidha, alipongeza juhudi za mkoa kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani katika ununuzi wa samani zilizohitajika katika Hospitali ya mkoa pamoja na chanagamoto kadhaa wanazokabiliana nazo.

“Global fund itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali, ninapongeza namna mkoa unavyokabili na kuboresha maeneo yaliyo na changamoto, kwa hapa Nzega jengo la maabara linaendelea vizuri lipo hatua za mwisho na lenye viwango vizuri hivyo thamani ya fedha zilizotolewa zinasadifu,”alisema Dkt. Rachel
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Crispin Musiba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu aliyoambatana nayo wakati wa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) mara baada ya kikao cha pamoja katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Akizungumzia ziara hiyo, Dkt. Rachel amesema,imelenga kutembelea mikoa sita ikiwemo wa Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Singida na Dodoma ikiwa ni miongoni mwa mikoa inayotekeleza miradi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news