Dkt.Gustavus Deusdedith aunga mkono maono ya Rais Dkt.Samia kupitia kiwanda cha nguo Taven

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji wa Taven Industries Company Limited,Dkt.Gustavus Deusdedith amesema, nia ya kuanzisha kiwanda hicho ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa nguo za aina mbalimbali nchini ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Kiwanda hicho kilichopo Block D, Plot 716, Chihoni Kata ya Nala jijini Dodoma,licha ya kuunga mkono jitihada hizo kimetoa fursa za ajira kwa Watanzania mbalimbali.

"Nia nzima ya uanzishwaji wa kiwanda hiki cha nguo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita hasa katika Sera ya Viwanda na hivyo kuongeza upatikanaji wa bidhaa hapa hapa nchini na sio kutoka nje ya nchi.

"Tunaunga mkono Serikali yetu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sera ya uzalishaji ambayo imekuwa ikinadiwa kwa miaka kadhaa. Sasa nasi, tumeona tuingie katika eneo hilo,"amefafanua Dkt.Deusdedith.

Akizungumzia kuhusiana na uzalishaji kiwandani hapo,Mkurugenzi Mtendaji huyo amefafanua kuwa,wanajihusisha na uzalishaji wa nguo za mitindo tofauti na aina mbalimbali hasa zile za mitindo ya kiofisi na kijamii.

"Tunazalisha zaidi tisheti na unifomu na mitindo mbalimbali inayoibuka kulingana na mahitaji.Tunazo aina tatu za tisheti zipo zenye shingo zina kola ni maarufu sana kwa jina la form six, tunazalisha pia zenye shingo ya mviringo na pia zenye shingo zenye alama ya V.

"Katika uzalishaji wa tisheti tuna uwezo wa mkubwa sana tunaweza kuzalisha hizi zenye kola takribani tisheti 5,000. kwa saa 12.

"Na hizi ambazo za raundi uzalishaji wetu unaenda mpaka tisheti 6,000. Ndani ya saa 12 na hizi ambazo zenye muundo wa shingo na alama V pia.

"Pia tunazalisha unifomu za aina mbalimbali, unifomu za biashara kama za benki, pia mashuleni vyombo vya ulinzi, lakini pia hata mahitaji ya walinzi binafsi sawa sawa na wale wanaolinda mabaunsa katika mitindo mingine.

"Tunazalisha kulingana na mahitaji ya wakati huu, mitindo ya akina dada, watoto, maharusi zote tunaweza kuzitengeneza kulingana na mahitaji ya mteja.

"Tunaweza kupokea sampuli kutoka kwa mteja au mchoro wa nguo anouhitaji yenye kitambaa cha asili tofauti kutokana na pamba, nailoni au mchanganyiko wa malighafi tofauti tofauti. Tunatengeneza kulingana na mahitaji yake.

"Tunafanya pia uchapishaji wa tisheti kwa njia tofauti tofauti kwa kudarizi, kuchapa kwa wino wa moto na njia nyingine za kitaalamu.Tunawakaribisha wateja wanaohitaji nguo na uchapishaji wa picha kwa mitindo mbalimbali katika kiwanda chetu.Kwa mawasiliano zaidi tunapatikana kwa namba 0717 514324 au 0786407282,"amefafanua Mkurugenzi Mtendaji wa Taven Industries Company Limited, Dkt.Gustavus Deusdedith.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news