Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, Mohamed Hassan Moyo amepiga marufuku taasisi na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kujishughulisha na mapenzi ya jinsia moja na ushoga.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na taarifa na mashirika yasiyo ya serikali, Moyo alisema kuwa hataki kusikia kuna shirika linapata fedha mahali kwa ajili ya kuhamasisha ushoga na ndoa za jinsia moja kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.