Jumla ya hekari 953 za mashamba ya bangi zimeteketezwa mkoani Arusha katika operesheni iliyofanyika kwa siku nane mkoani humo kuanzia Mei 31 hadi Juni 7, 2023 ikilenga kukabiliana na kilimo cha bangi.
Bangi hizo zimeteketezwa zikiwa bado mbichi shambani ambapo kulingana na makadirio yaliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) ni sawa na gunia 4,765.