“Kwa namna ya kipekee kabisa napenda kumpongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kuleta hamasa kwa timu zetu katika michezo ya Kimataifa kwa kununua kila goli linalofungwa na timu zetu zinapokuwa katika mashindano ya Kimataifa ambapo kutokana na juhudi hizo timu ya Simba imepata shilingi milioni 55 na Yanga shilingi milioni 135, Yanga hoyeee,"Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba Juni 15, 2023 wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya Hali ya Uchumi wa Kitaifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2023/2024.