Katika hatua nyingine, Kampuni ya Taifa Gas ya Tanzania imetangaza uwekezaji mkubwa nchini Zambia wa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi itokanayo na mafuta (LPG).Taifa Gas itashirikiana na Kampuni ya wazawa ya Delta Marimba Limited kuzalisha megawati 100 za umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya Taifa nchini Zambia.
Makubaliano hayo yametangazwa na pande hizo mbili Juni 26, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas, Hamis Ramadhan amesema, kampuni hiyo itakuwa ya kwanza ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi ya LPG na mradi huyo utatekelezwa nchini Zambia.