Serikali imesema imefanya jitihada kubwa ya kupunguza changamoto za biashara nchini hususani kupunguza utitiri wa tozo kutoka 380 hadi 148 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2020/2021.Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande ameyasema hayo Juni 28, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Buhigwe, Kavejuru Felix (CCM). 
