Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeachana na kipa wake nne, Erick Johola baada ya misimu miwili tangu awasili Jangwani akitokea Aigle Noir ya Burundi. Johola anakuwa mchezaji wa sita kuachwa Yanga baada ya beki, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC, mawinga Mghana, Bernard Morrison, Mkongo Tuisila Kisinda na mzawa, Dickson Ambundo. Pia, Yanga SC imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov na kuajiri Kocha mpya, Muarngentina Miquel Angel Gamondi.