Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 5, 2023 ameialika timu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) kwa chakula cha jioni Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo kuipongeza kwa kufanya vizuri katika michuano ya soka ya kugombea Kombe la Shirikisho Barani Afrika iliyohitishwa juzi jijini Algers, Algeria.