Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameitaka Klabu ya Yanga kumaliza mgogoro na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’. Ametoa agizo hilo Juni 5, 2023 katika hafla ya chakula cha jioni ya kuwapongeza Yanga kwa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Juni 3,2023 dhidi ya US Alger ya Algeria."Sifurahi migogoro kati ya viongozi na wachezaji, issue ya Fei Toto mkaimalize.Haipendezi klabu kubwa kama hii kuwa na ugomvi na mtoto mdogo, hebu kamalizeni, kisha mje nyumbani kunieleza.”