Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewakamata watuhumiwa watano wa unyang’anyi kwa tumia silaha ambao kati yao wawili wametambuliwa kuhusika katika tukio la ubakaji alilofanyiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa (jina linahifadhiwa) wakati wakifanya uharifu chuoni hapo. Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema watuhumiwa hao walikamatwa hivi karibuni wakiwa na mapanga matatu, praiz mbili na bajaji namba MC 206 DFF waliyokuwa wakiitumia kufanya uhalifu katika chuo hicho, Semtema, Mkwawa na Mtwivila mjini Iringa.