Kiungo mpya wa Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto, amesema anafuraha kubwa sakata lake na waajiri wake wa zamani Yanga SC kumalizwa na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulimaliza sakata hilo.“Ninamshukuru Rais kwa kulimaliza hili jambo, nitazidi kumuombea katika majukumu yake.Nawashukuru pia mashabiki wa Yanga na viongozi kwa upendo walionionesha.”