Halmashauri zapewa fursa mpya ya kununua nyumba za NHC

NA MWANDISHI WETU

HALMASHAURI nchini ambazo maeneo yao zimejengwa nyumba za gharama nafuu na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zimepewa fursa ya kununua nyumba hizo kwa mfumo wa mpangaji mnunuzi. 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC wilayani Mkinga leo.

Fursa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah alipozungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Kanali Maulid Surumbu alipofika kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC wilayani humo.

Akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanali Maulid Surumbu alipofika kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC wilayani humo, Bw.Hamad Abdallah ameeleza kuwa, utaratibu huo unawezesha halmashauri kuwa na maelewano ya muda mrefu na NHC yatakayowezesha watumishi wa halmashauri kulipia nyumba hizo kwa muda wa miaka mitano hadi kumi na baadae kodi yao kuhesabika kama sehemu ya manunuzi ya nyumba wanazopanga.
Utaratibu huo ulipokelewa kwa shauku kubwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye alibainisha kuwa kwa sasa wilaya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 ina mahitaji makubwa ya nyumba yaliyotokana na uwepo wa taasisi nyingi za serikali na binafsi ambazo hazina makazi ya uhakika. 
Pia amesema kuwa,wilaya hiyo iliyopo mpakani mwa Kenya ina fursa nyingi za kitalii na imepewa hadhi na Mkoa wa Tanga kuwa Wilaya ya kimkakati katika kuvutia utalii wa ukanda wa Pwani wa mkoa huo. 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah akiwa na kikao na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Bi.Zahra Msangi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bi.Zahra Msangi amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa NHC kuwa wataishauri Serikali kuruhusu fedha inazotenga kwa ajili ya nyumba za watumishi wake zitumike kununua nyumba za NHC zilizojengwa katika wilaya hiyo. 
Mkurugenzi huyo ameikaribisha NHC kufanya mazungumzo yatakayowezesha halmashauri hiyo kununua nyumba hizo na kwamba kwa kuanzia atahakikisha watumishi wa halmashauri wanaopanga katika nyumba hizo wanalipa kodi kwa wakati. 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Kanali Maulid Surumbu akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Kanali Maulid Surumbu alipofika kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC wilayani humo.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah alikuwa katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na NHC katika Mkoa wa Tanga na kuhimiza utendaji kazi kwa watumishi wa Shirika hilo ili kuongeza tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news