ARUSHA-Jopo la majaji saba lililokaa Bagamoyo mkoani Pwani kwa siku tisa kuanzia Juni 10 – 18, 2023, kupitia kazi 893 zilizowasilishwa kwa ajili ya mashindano ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2022, limekamilisha kazi yake kwa kupata wateule 91.
Jopo hilo lilitumia siku tisa badala ya nane kutokana na ongezeko la kazi 295 kutoka kazi 598 za EJAT 2021. Hapa niwapongeze na kuwashukuru majaji kwa kazi kubwa waliyoifanya kupitia kazi hii.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tuzo hizi, waandishi wa habari walituma kazi zao kwa njia ya mtandao hali ambayo imerahisisha kazi kwa majaji na Sekretariati. Baraza litaendelea na utaratibu huo katika Tuzo zijazo.
Safari hii jumla ya waandishi 91 wameteuliwa kati ya waandishi 728 waliowasilisha kazi zao. Kati ya hao, 36 wanaandikia magazeti, 27 mitandao ya kijamii (Online) na 15 kutoka radio wakati wanaotokea kwenye runinga walikuwa 13.
Pia kati ya wateule hao, 44 ni wanawake ambapo 16 ni kutoka kwenye magazeti, 12 kutoka mitandao ya kijamii na sita kutoka radio na runinga ni 10. Wateule wanaume ni 47, ambao 20 wanaandikia magazeti, 10 ni waandishi wa radio na runinga ni saba, ambapo mitandao ya kijamii ilikuwa na waandishi 10.
Katika Tuzo za mwaka juzi yaani EJAT 2020, jumla ya waandishi 59 waliteuliwa kuingia katika hatua hii, ambapo EJAT 2021 waandishi wa habari 60 waliingia katika kinyang’anyiro hicho.
Jopo la Majaji liliongozwa na Mkumbwa Asaad Ally. Majaji wengine ni Mwanzo Lawrance Millinga, Peter Wallace Nyanje, Mbaraka Abdi Islam, Dk, Egbert Emmanuel Mkoko, Rose Haji Mwalimu, na Nasima Haji Chum.
Washindi wa tuzo hizo watajulikana rasmi katika kilele cha Tuzo za EJAT 2022 zitakazofanyika Julai 22, 2023 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Haki Jinai.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT ni Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambalo ni Mwenyekiti, Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Habari ya Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), HakiElimu, ANSAF, na SIKIKA.

Makundi yaliyoshindaniwa ni :
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Data;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu na Watu;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Watu wenye Ulemavu;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya;
- Tuzo ya Uandishi wa Sayansi na Teknolojia;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Ushirika;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Kodi, Tozo na Mapato;
- Tuzo za Uandishi wa Habari za Sensa;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya Maji;
- Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Uzazi
- Kundi la Wazi;
SN JINA LA MTEULE CHOMBO MKOA
1 Ephrahim Bahemu Mwananchi Dar es Salaam
2 Peter Elias Mwananchi Dar es Salaam
3 Shabani Njia Hamisi Nipashe Shinyanga
4 Flora Primo Siriwa Moshi FM Kilimanjaro
5 Elizabeth Kilindi Nipashe Njombe
6 Jackline Silemu ITV Dar es Salaam
7 Salumu Vuai Issa Zanzibar Leo Zanzibar
8 Rahma Suleiman Ali Nipashe Zanzibar
9 Hermina Emil Mkude Nukta Africa Dar es Salaam
10 Haji Nassoro Mohammed Zanzibar Leo Pemba
11 Anthony Mayunga Jamhuri Mara
12 Faraja Benedict Masinde Gazetini Dar es Salaam
13 Mohammed Makonda Radio Kwizera Kagera
14 Catherine Madabuke Mazingira FM Mara
15 Hamisi Makungu Hamisi Pangani FM Tanga
16 George Henry Helahela The Citizen Digital Dar es Salaam
17 Hazla Omary Quire TSN digital Dar es Salaam
18 Julius Mathias Mnganga Mwananchi Dar es Salaam
19 Mussa Juma Siwayombe Mwananchi Arusha
20 Ramadhani Kabanga Mvungi Azam TV Arusha
21 Naishooki Alais Makeseni Star TV Dodoma
22 Issa Juma Ramadhani Dar24 Dar es Salaam
23 Elizabeth Edward Kusekwa Mwananchi Dar es Salaam
24 Warioba Igombe Warioba Uhuru Morogoro
25 Vumilia Alex Macha Savvy FM Arusha
26 Tumaini Godwin Msowoya Mwananchi Iringa
27 Imani Henrick Luvanga Kings FM Njombe
28 Nicolaus King Mwanalus Wasafi TV Dar es Salaam
29 Vicky Ebeneza Kimaro Habari Leo Dar es Salaam
30 Ezekiel Hassan Shamakala TBC Taifa Dar es Salaam
31 Omary Hussein Omary Star TV Morogoro
32 Khamisuu Abdallah Ali Zanzibar Leo Zanzibar
33 Mukrim Mohamed Khamis KTV TZ Online Zanzibar
34 Haika Kimaro Habitat News Mtwara
35 Adella H. Tillya Wasafi FM Dar es Salaam
36 Harith Jaha Ally Watetezi TV Mwanza
37 Alex Selestine Kazenga Jamhuri Dar es Salaam
38 Imani Raphael Makongoro Mwananchi Dar es Salaam
39 Najjat Haji Omar The Chanzo Zanzibar
40 Lukelo Francis Haule The Chanzo Dar es Salaam
41 Saddam Sadick Mayala Mwanasport Dar es Salaam
42 Fatuma Mtemangani Radio Ulanga FM Dar es Salaam
43 Josephine Sebastian The Citizen Mwanza
44 Manyerere J. Nyerere Jamhuri Dar es Salaam
45 Albuni Albuni Mwedadi Mlimani Radio Dar es Salaam
46 Lucy Patrick Samson Nukta Africa Dar es Salaam
47 Juma Mussa Issihaka Mwananchi Dar es Salaam
48 Warioba Igombe Warioba Uhuru Morogoro
49 Yusra Said Shaaban RSV Online TV Zanzibar
50 Protte Profit Mmanga Leo TV online Arusha
51 Amina Salum Kasheba Uhuru Dar es Salaam
52 Joseph Kirati Kirati The Chanzo Dar es Salaam
53 Alfred Lasteck Mushi BBC Swahili Dar es Salaam
54 Mariam Shaban Mbwana Mwananchi Dar es Salaam
55 Heneliko Leonard Malo Bomba FM Iringa
56 Kelvin Paul Matandiko Mwananchi Dar es Salaam
57 Abel Claud Kilumbu Dar24 Dar es Salaam
58 Mwajuma Hassan Rajab EATV Dar es Salaam
59 Jackline Victor Kuwanda The Chanzo Dar es Salaam
60 Herieth Makwetta Mwananchi Dar es Salaam
61 Sanula Athanas Nipashe Dar es Salaam
62 Daniel Mwalubuli Nukta Africa Dar es Salaam
63 Pamela Nesphory Chilongola Mwananchi Dar es Salaam
64 Khadija Ali Yusuph Radio Jamii Mkoani Zanzibar
65 Cosmas C. Mwamposa Pangani FM Tanga
66 Francis Dhamira Kajubi The Guardian Dar es Salaam
67 Asifiwe Brown Mbembela The Chanzo Mbeya
68 Janet Kimario Joseph Mwananchi Kilimanjaro
69 Said Ally Sindo Storm FM Geita
70 Ayoub Stanley Nyondo Shamba FM Iringa
71 Anna Peter Mbuthu TBC1 Dar es Salaam
72 Daniel Hezron Limbe Malundeblog Geita
73 Stanslaus Bernard Lambart Dar24 Dar es Salaam
74 Zuhura Hassan Makuka Dar24 Dodoma
75 Anna Thadei Augustino EATV Arusha
76 D’jaro Deus Arungu TBC FM Dar es Salaam
77 Baraka Mnyalei Loshilaa Mwananchi Dar es Salaam
78 Festo Charles Lumwe Dar24 Dar es Salaam
79 Peter Lugendo John TBC Taifa Dar es Salaam
80 Dafrosa Prosper Ngailo Azam TV Dar es Salaam
81 Zuhura Juma Said Zanzibar Leo Zanzibar
82 Elesia Thomas Haule Azam TV Dar es Salaam
83 Suleiman Omary Mwiru Nukta Africa Dar es Salaam
84 Adam Gabriel Hhando CG FM Tabora
85 Grace Elibariki Mbise Star TV Mwanza
86 Ahmadi Ally Mramba TBC1 Dodoma
87 Heldina G. Mwingira Dar24 Dar es Salaam
88 Augusta Mathias Njoji Nipashe Dodoma
89 Clezencia Tryphone Mwanasport Dar es Salaam
90 Dauka Abraham Somba Dar24 Dar es Salaam
91 James Daud Lerombo TBC1 Mwanza
Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi EJAT 2022