Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na baadhi ya wabunge baada ya kusoma hotuba ya kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Juni 28, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na baadhi ya wabunge baada ya kusoma hotuba ya kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Juni 28, 2023. Amesema, Serikali itahakikisha kuwa, mikataba ya utekelezaji wa makubaliano ya uendeshaji wa maeneo ya bandari nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World itazingatia maslahi ya nchi na kuleta manufaa kwa Taifa letu.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa makubaliano yaliyoingiwa yanalenga kuweka msingi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai. Pia, amezielekeza halmashauri zote nchini zihakikishe maeneo yote yanayotwaliwa kutoka kwa wananchi yanalipiwa fidia kwa wakati ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza siku za usoni.