Hospitali ya Benjamin Mkapa yapandikiza uume kwa mara ya kwanza nchini

NA MWANDISHI WETU

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH)kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo nchini (TAUS) pamoja na daktari bingwa kutoka Ufaransa kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupandikiza uume kwa watu wawili ambao uume ulishindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa mbalimbali.
Akizungumza baada ya kukamilisha upasuaji huo, Dkt. Remidius Rugakingira daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na wanaume kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa amesema kuwa, upasuaji huu umefanyika kwa mara ya kwanza nchini.

“Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya upasuaji wa aina hii kilichofanyika hapa ni kuweka vipandikizi maalumu vitakavyowezesha uume kurudi katika hali yake upasuaji huu tumeshirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo pamoja na daktari bingwa wa mfumo wa mkojo kutoka Ufaransa na tumefanikiwa katika hilo,”ameeleza Dkt.Rugakingira.

Dkt. Rugakingira aliendelea kwa kusema kuwa, huu ni wito kwamba Hospitali ya Benjamin Mkapa inajali afya ya wanaume na upasuaji kama huu unaweza kufanyika Tanzania.

Kwa upande wake Dkt.Liuba Nyamsogolo ambaye ni kiongozi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo (TAUS) amesema kuwa, wamefikia hatua hii kutokana na uwepo wa watu wengi wenye matatizo ya nguvu za kiume nchini na Afrika kwa ujumla.

“Moja wapo ya dhumuni ya TAUS ni kuendeleza wataalam nchini kwa kushirikiana ma wataalam kutoka nje ili kuleta teknolojia inayopatikana duniani nchini Tanzania na kutibu magonjwa kama haya kwa wale wenye matatizo,” amesema Dkt. Nyamsogolo.
Msemaji wa BMH,Bw. Jeremiah Mbwambo ameeleza, "Hospitali ya BMH imekua hospitali ya kwanza nchini kufanya upasuaji wa kuweka vipandikizi kwenye uume kwa wagonjwa wenye matatizo ya nguvu za kiume, serikali ya awamu ya sita imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuiwezesha teknolojia za kisasa za matibabu ili kuwapatia matibabu thabiti wananchi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news