Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) yakaribisha wadau kuchangia damu

NA MWANDISHI WETU

KUELEKEA siku ya mchangia damu duniani ambayo huadhimishwa Juni 14 ya kila mwaka, Hospitali ya Taifa Muhimbili U(panga na Mloganzila) jijini Dar es Salaam imewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchangia damu katika vituo vyao vya damu salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amewaomba wananchi kufika kwenye vituo hivyo ambapo huduma zinatolewa kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni.

"Kwa siku moja, mahitaji ya damu ni chupa/ unit 120 hadi 150, hata hivyo makusanyo yetu kwa siku ni chupa 60 hadi 80 tu, hivyo kufanya hospitali kuwa na upungufu kwenye benki ya damu kila siku.

"Wachangiaji wafike jengo la Maabara Kuu, Kitengo cha Damu Salama ambapo kinatazamana na jengo la Magonjwa ya Dharulr (Emergency Medicine),"amesema.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ikihudumia watu mbalimbali wa nje na ndani, hivyo mahitaji ni makubwa ya damu kwa kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news