Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Camillus Wambura akimjulia hali Askari Polisi PC Emmanuel Kundi wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha Juni 9,2023 kwa ajili ya kumuona Askari huyo aliyepata ajali ya kugongwa na pikipiki Juni 3, 2023 mkoani Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Camillus Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Polisi Mkoa wa Arusha mara baada ya kufanya kikao kazi cha Maelekezo kilichofanyika katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani humo Juni 09, 2023. Katika kikao hicho amewataka Maafisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na Tanzania isiyokua na uhalifu.