NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amewakumbusha watumishi wa ofisi yake kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuyafikia malengo ya Serikali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt. Jim Yonazi akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao chake na wafanyakazi wa Ofisi yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 23, 2023. Kikao kilifanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Njedengwa jijini Dodoma.(Picha na OWM).
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao chake na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 23, 2023.
Katibu Mkuu huyo amesema, upo umuhimu wa kujizoeza kupima afya hususani kwa magonjwa sugu yasiyoambuiza kwani yameendelea kuwa changamoto hasa kwa watu wenye umri mkubwa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt. Jim Yonazi akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao chake na wafanyakazi wa Ofisi yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 23, 2023. Kikao kilifanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Njedengwa jijini Dodoma.(Picha na OWM).
“Ni muhimu tumepata fursa ya kukumbushwa kupima afya zetu, hii ni changamoto inayotukabili, hivyo ni muhimu kuzingatia ushauri wa afya na masharti ya namna ya kuboresha masuala yanayohusu afya zetu,"amesema Dkt.Yonazi.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao jijini Dodoma.
Pamoja na hilo aliwakumbusha watumishi kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ili kuendelea kutekeleza majukumu wakiwa wenye afya na kuwa na matokeo chanya.
Aidha, aliutumia mkutano huo kuwaasa watumishi hao kuongeza ubunifu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku huku wakizingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao jijini Dodoma.
“Mkutano huu ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo tulianza kuiadhimisha tarehe 16 Juni, 2023 na leo ndio kilele.
"Wiki hii tunaitumia kutafakari namna tunavyotekeleza majukumu yetu kwa kipindi kilichopita, kujadili namna ya kutoa huduma bora kwa jamii ya Watanzania, kujifunza mbinu mpya na kuibua changamoto zinazotukabili katika kutekeleza majukumu yetu kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi,”alisisitiza.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamilzi wa Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Bi.Stella Mwaiswaga (wa kwanza kushoto waliokaa) na kulia ni Bi. Numpe Mwambenja, Mwenyekiti wa TUGHE wa Ofisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma.
Pia aliwahimiza Watumishi kuendela kufanya kazi kwa upendo na kuheshimiana kwani kwa kufanya hivyo wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa amani.
“Ni falsafa yangu kuona watu ninaowaongoza wanafanya kazi kwa upendo na kushirikiana, ni lazima kuhusiana na kuwa na mashirikiano mazuri, napenda kufanya kazi na watu wanaoheshimiana na wenye amani siamini kama mtu anaweza akafiri vizuri iwapo hana amani ndani,”alisisitiza Dkt.Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamilzi wa Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Bi.Stella Mwaiswaga (wa kwanza kushoto waliokaa) na kulia ni Bi. Numpe Mwambenja, Mwenyekiti wa TUGHE wa Ofisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamilzi wa Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Bi.Stella Mwaiswaga (wa kwanza kushoto waliokaa) na kulia ni Bi. Numpe Mwambenja, Mwenyekiti wa TUGHE wa Ofisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma.
Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Numpe Mwambenja alipongeza uwepo wa mkutano huo huku akieleza kuwa ni nyenzo muhimu kwa kuongeza motisha kwa watumishi wa umma, na imeonesha kujali na kuendelea kuleta umoja kazini.
“Mkutano huu umekuja wakati sahihi na muda sahihi, tunawapongeza viongozi wetu kuendelea kutuweka pamoja na kutukumbusha kupendana, kushirikiana na kuishi kwa amani, hili tumelithamini sana na tunaahidi hatuta waangusha tutachapa kazi na kuendele kuhudumia jamii ya Watanzania na kuitumikia nchi yetu kwa ujumla,”alisema Numpe.