Konseli Kuu ya Lubumbashi yakutana na madereva

NA MWANDISHI WETU

KAIMU Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa akiwa na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala walifanya ziara ya kutembelea madereva wa malori ya Tanzania yanayofanya safari kati ya Tanzania na DRC upande wa Jimbo la Haut-Katanga na Jimbo la Lualaba. 
Madereva wa Malori wakielezea changamoto wanazokutana nazo na kupewa majibu kutoka kwa Wahusika.
Kaimu Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwasili eneo la kuegesha malori kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo madereva wa Tanzania wanaofanya safari kati ya Tanzania na DRC.

Ujumbe huo uliofika maeneo hayo tarehe 12 Juni 2023 ulisikiliza changamoto za kiusalama zinazowakabili madereva wa malori wanaosafirisha mizigo kati ya DRC na Tanzania inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam. Mhe. Ndala aliahidi kuendelea kuboresha hali ya usalama wa madereva na mizigo akitoa mfano wa mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza vitendo vya utekaji wa malori yanayobeba madini ya shaba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news