Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ndege mpya ya mizigo aina ya BOEING B767-300F katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam -Terminal One leo Juni 3, 2023;
Ndege hiyo ya mizigo ambayo ni ya kwanza kununuliwa Tanzania inatarajiwa itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara waliokuwa wanakumbana na changamoto za usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi na kulazimika kutumia nchi jirani ambako gharama huwa juu.
Ununuzi wa ndege hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuimarisha utendaji kazi wa ATCL ambapo kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa, tayari malipo ya awali kwa ajili ya ununuzi wa ndege mbili za Boeing 737-9, ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400, na ndege moja Boeing 787-8 yameshafanyika.