NA ADELADIUS MAKWEGA
WANACHUO wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya–Kwimba mkoani Mwanza wamemuomba Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania asimuhamishe kituo cha kazi Kaimu Mkuu wa jeshi hilo wilayani Kwimba, SGT. Regina Jackson Mhindilo kwani amekuwa akifanya kazi yake kwa uhodari ya kutoa elimu ya Zimamoto na Uokoaji na kwa ustadi mkubwa kwa wananchi wa vijiji vyote wilayani Kwimba bila ya kuchoka.
Hayo yamesemwa kandoni ya mafunzo yaliyotolewa na SGT Regina (ZM 2835) katika viwanja vya Chuo hiki na Rais wa Serikali ya Wanachuo Baptist Kapinga ambapo ZM 2825 alitumia muda wa saa karibu tatu kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo yaliwavutia mno wanachuo hao.
“ZM 2835 amemwakilisha vizuri mkuu wa Jeshi Zimamoto na Uokoaji nchini, mama tunakupa pongezi kwa kazi nzuri, pongezi kwa Mkuu wa Zimamoto lakini tunamuomba asikuhamishe Kwimba, ubaki hapa hapoa kutuhudumia na pia tunaomba namba yako ya simu tukiwa na lolote tuwasiliane nawe.”
Naye ZM 2835 hakuwa na hiana alitoa namba mbili binafsi na ya huduma kwa wateja simu ya bure 114.
Wakiwa katika mafunzo hayo wanachuo hao walipata nafasi za kuuliza maswali mbalimbali ambapo Christopher Sodike aliuliza suala milango mingi ya taasisi inashauriwa kufunguliwa kwa nje, kwa nini milango mingine yote isifunguliwe kwa nje? Huku mkurufunzi Sodike akikumbusha tukio la kuungua mabweni shule ya sekondari Idodi Iringa vijijini iliyosabbaisha vifo vingi ambapo ndugu Sadoki alisema alikuwepo mdogo wake ambaye alijua kidogo kichwani lakini alikutwa mzima.
“Milango ya umma inashauri kufunguliwa kwa nje lakini katika kila nyumba zetu binafsi tunashuriwa kuwe na mlango mmoja wa dharura, huo utatumika kukitokea tukio la ajali ya Zimamoto na Uokoaji .”
Alisema Kaimu Mkuu wa Zimamoto wilaya ya Kwimba. Kwa upande wake mkurufunzi Amina Shabaan aliuliza kwa nini inalazimishiwa milango ya taasisi kufunguka kwa nje badala ya ndani?
“Milango inayofungua kwa nje, wakati wa taharuki inakuwa miepesi kufunguka, kwa haraka kuliko ile inayofunguliwa kwa ndani, huku ikisisitizwa milango hiyo inayofunguka kwa nje iwe milangoya mbao tu isiwe ya bati au chuma kwa maana wakati wa ajali milango ya bati/ chuma inakuwa ngumu kufunguka kwa urahisi.”
Akizungumza kandoni mwa mafunzo hayo Makamu Rais wa Serikali ya wanachuo Bi Maria Mshani amesema kuwa anashauri kila pahala kilipo Kituo cha Polisi Tanzania wawepo askari wa Zimamoto na Uokoaji wawili kwa kuanzia wakati tukisibri maboresho ya jeshi hilo nchni nzima.
Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Chuo cha Manendeleo ya Michezo, Richard Mganga alitoa tahadhari kwa wanachuo wake kutunza mali za umma ikiwamo mitungi ya Zimamoto ya uokoaji ili kuwa mizima panapotokea ajali ifanya kazi yake iliyokusudiwa.
Mwandishi wa ripoti hii alishuhudia wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya wakiume wakihifadhi namba ya simu ya Kaimu Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kwimba ZM 2635, huku wanachuo wasichana wakisema, “Haya jamani kaka zetu namba mmepata, kazi kwenu.” huku wanachuo wavulana wakisema ajali ya moto haina mvulana wala msichana.