Mandonga atambulisha ngumi mpya ya Kingugi

NA ELEUTERI MANGI-WUSM

BONDIA Machachari,Bw. Karim Said maarufu Mandonga Mtu kazi ametembelea banda la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo ametangaza ngumi mpya iitwayo "Kingugi" anayotarajia kuitumia kwenye mchezo wa marudiano na Bondia Daniel Wanyonyi kutoka Kenya. 
Mandonga ametangaza ngumi hiyo Juni 29, 2023 kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa Sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Mandonga ameishukuru Serikali kwa kusimamia vema michezo hatua iliyomfanya ajulikane kimataifa na kuhamasisha vijana kupenda michezo ili kuendesha maisha yao.
Akimkaribisha bondia Mandonga Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo ya 2023, Bi.Zahara Guga amesema Wizara ni mlezi wa masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hivyo, Mandonga ni miongoni mwa Wadau wake yupo kwenye ofisi yake ya kazi.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imejikita kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuhamasisha wadau hao kurasimisha kazi zao ambazo ni ajira ya kujipatia kipato kwa kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news