Miamala shuku 769, taarifa fiche 314 zafikishwa ngazi husika

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (MB) amesema, katika mwaka 2022/23,Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu kilipanga kupokea na kuchambua miamala ya fedha na kuandaa taarifa fiche kwa hatua stahiki.

Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo Juni 7, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bungeni Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2023/24.

"Hadi Aprili 2023,kitengo kimepokea taarifa 7,313 za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi trilioni 56.65, taarifa 8,784 za usafirishaji fedha kwa njia ya kielektroniki zenye thamani ya shilingi trilioni 222.81 na taarifa 2,457 zinazohusu usafirishaji wa fedha taslimu na hati za malipo kupitia mipakani.

"Aidha, kitengo kimechambua miamala shuku 769 na kuandaa taarifa fiche 314 na kuwasilisha kwenye taasisi za utekelezaji wa sheria kwa hatua za uchunguzi,"amefafanu Waziri Dkt.Mwigulu.

Vilevile, amesema mfumo wa kitengo hicho umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar pamoja na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili kusomana na kubadilishana taarifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news