Mihemko ya ushindi changamoto kwa waamuzi

NA ADELADIUS MAKWEGA 

CHANGAMOTO wanazopata waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu zinatokana na wachezaji, viongozi wa timu waliopo uwanjani kuwa na mihemko ya kuutafuta ushindi katika mechi mbalimbali ziwe za Kitaifa hata Kimataifa.
Hayo yamesemwa Juni 14, 2023 na mkufunzi mwandamizi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Omari Rashidi Mataka ambaye pia ni muamuzi Daraja la Kwanza wa mchezo huo hapa Tanzania. 

Akiwa katika kiwanja cha mchezo huo hapa Malya, Kwimba-Mwanza, akizungukwa na kundi la wakurufunzi wa michezo wanaokaribia 100, mkufunzi Mataka alisema kuwa waamuzi wanapambana na changamoto nyingi uwanjani na ndiyo maana chuo cha Malya kilianzisha kutoa mafunzo na uamuzi wa mpira wa miguu ili wanaohitimu kuwa na mbinu za kuchezesha mchezo huo vizuri, kupunguza changamoto hizo na kuwapa burudani watazamaji wa mchezo huu wenye mashabaki wengi ulimwenguni. 
“Ninafundisha katika ngazi ya Astashahada na Stashahada, sasa nimeshamaliza kufundisha sheria namba tano ambayo ni matumzi ya filimbi na sasa ninafundisha sheria namba sita hasa waamuzi wasaidizi wakiwa kazini. Hapa ni sheria namba tano na sheria namba sita kwa pamoja namna zinavyoshirikiana kufanya maamuzi mbalimbali kiwanjani.” 
Akiendelea kufundisha somo hilo kwa umahiri mkubwa huku milio kadhaa ya filimbi ikisisika ambayo ilimpa ishara kila aliyekuwepo hapo kutambua kuwa hapo kweli na hakika somo la Uamuzi wa Mpira wa Miguu likifundishwa.

Mwisho mwa kipindi hicho mkufunzi Mataka alitoa nafasi wa wakurufunzi wake kuuliza maswali ambapo hilo lilimpa nafasi hata kufanya tathmini ya somo lake ndani ya dakika 120 ambapo somo hilo lilifanyika huku kukiwa na manyunyu kidogo na baridi kiasi na hali hiyo kuwavutia mno wakurufunzi hao. 
“Mimi nina ushauri, kuna baadhi yetu ni waoga, wanaogopa mno, unakuta mtu amekwenda kwenye filimbi, anaogopa kwenda kwenye kibendera. Jamani mimi ninaona hakuna haja ya kuogopa.” Haya yalisemwa na mkurufunzi Rahama Simba anayesoma Astashahada ya Michezo.
Tathmini hiyo ilihitimishwa na mkurufunzi Said Kasana ambaye alimpongeza zaidi mkufunzi Mataka kwa kutokuwa mkali katika somo hilo akisema kuwa somo lake limeeleweka mno naye mkufunzi akisisitiza kuwa ukali wake mafunzoni anatumia kujenga umakini na kuhakikisha kila mkurufunzi wake anayefunza ajenga kujiamini na aweze kuhimili mihemko ya wachezaji viwanjani 
Mwandishi wa ripoti hii aliyeshuhudia dakika zote 120 za somo hilo amejifunza kuwa panapochezeshwa mpira wa miguu muamuzi wa kati hatakiwa kuiweka mdomoni filimbi muda wote, bali ni wakati tu pale anapopiga filimbi hiyo tu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news