Mito yote Morogoro, Hili ndilo ghala letu

NA LWAGA MWAMBANDE

MKOA wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa nchini ambao umejaliwa kuwa na mito na mabwawa yenye samaki wengi.

Sehemu kubwa ya uvuvi hufanyika kutokea kwenye kambi za wavuvi kandokando ya mto Kilombero. Kuna aina zaidi ya 52 ambapo zaidi ya asilimia 90 ya samaki wote wanapatikana kutokea mto Kilombero.

Uvuvi mwingine kwa kiwango kidogo hufanyika katika mabwawa ya asili, ya kuchimbwa na mito imwagayo maji yake katika bonde la mto Rufiji. Kutokana na vyanzo hivyo vyote, kila mwaka mkoa unakadiriwa kuzalisha samaki zaidi ya tani 350.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema licha ya fursa za uvuvi, pia mito hiyo imeendelea kuwa neema kwa ajili ya shughuli za kilimo,maji na ufugaji ambapo anakujatia mito hiyo. Endelea;


1.Morogoro ghala letu, tena utajiri wetu,
Mkoa chakula chetu, na chanzo cha maji yetu,
Huo ni wa nchi yetu, na rasilimali yetu,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

2.Iwe kilimo chakula, hili ndilo ghala letu,
Kwa biashara si jela, yalimwa mazao yetu,
Zinafaa Pawa Tila, hata kwa mifugo yetu,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

3.Wa kwanza mto Bwakira, uko mkoani kwetu,
Chemezi na Ifakara, nayo ina maji yetu,
Chigange na Mgambira, nayo yatunywesha kwetu,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

4.Chemezi Chigage Dete, Chiwa-Chiwa na Diwale,
Chogoali na Idete, Dogomi Gombo Liwale,
Chombohi Funga Kitete, Farua Kuli Lufile,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

5.Ibuti Londo Lidete, Hembwesa Lumba Mgawile,
Idaho Luri Kidete, Mbalu Jakulu Mulale,
Ihanga Nyama Rudete, kilimo kwa kwenda mbele,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

6.Ilongu Ihongolero, Kibirigu Kilakakala,
Ivimbi Mwega Mgera, Kayeyeya na Wysila,
Illongu Wundu Mnyera, Msegere na Msola,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

7.Kuna Little Msowera, Kilombero na Kirama,
Kibedya na Mtimbira, Kihanzi Kikalo Luma,
Kimamba na Mvomera, Luhembe Yovi Kisima
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

8.Kimbwe Lusongwe na Manga, Lubombero Luhangazi,
Kitalawe na Kiswaga, Langangulu Lubasazi,
Kisangata na Lukanga, Lukandi Yabo Mganzi,
Moto yote Morogoro, majina nakutajia.

9.Lukonde Tami Lukanga, Lukosi na Mohazima,
Lulongwe Lumeno Munga, Lumumwu Sofi Lumuma,
Lusesa Tami Majawanga, Luwegu na Niagama,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

10.Madukwa na Majawanga, Mafugusa na Maganga,
Malepeta na Mgonga, Matisi Sanje Mpanga,
Matuli Saso Mhanga, Ngulungulu na Mtega,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

11.Mbakana pia Matunda, Mchilipa na Mgata,
Mbakana mto Mdanda, Mhangasi na Mgeta,
Ruaha Mkuu penda, Mihangalaya Mkata,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

12.Mloui na Mkuzi, Melela pia Mihindo,
Mfumbu, Morogoro na Mitondo
Msumbisi na Mtega, Mgonya pia Ulondo,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

13.Miwasi na Mkondoa, ni mito haina kero,
Miyombo Mkundi poa, Mkubehi na Msoro,
Msumbisi maji toa, Mtshwege na Mswero,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

14.Mutimtali Mtumbe, Muhanga na Nakarsonde.
Mungako Mvuha Ngombe, Namawala Namingunde,
Mvumi Rudete Ruembe, Rufiri Ruipa Ngende,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

15.Mzelezi Nyambanitu, Namikoreko ni yetu,
Rufiri Ruhudji yetu, na Ruvumo mto wetu,
Suguta huo mto wetu, Na Sumbadsi ni wa kwetu,
Mito yote Morogoro, majina nakutajia.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news