NA LWAGA MWAMBANDE
MASHUJAA FC ya mkoani Kigoma imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City.
Picha haina uhusiano na mchezo wa Mashujaa FC dhidi ya Mbeya City.
Ni katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kucheza ligi hiyo msimu ujao uliofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
John Budeba dakika ya 87 ndiye aliyeiwaandikia historia Mashujaa FC kupitia bao pekee ambapo kwa kwa matokeo hayo wanapanda kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Ikumbukwe, Mashujaa FC walifikia hatua hiyo baada ya kuwatoa Pamba FC ya Mwanza waliokuwa nao Championship, wakati Mbeya City iliangukia hapo baada ya kutolewa na KMC waliokuwa nao Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara katika mechi za mchujo wa kwanza.
Aidha, hatua hiyo inathibitisha kuwa,msimu ujao wa ligi kutakuwa na wageni watatu kutoka Championship, mbali na Mshujaa nyingine ni mabingwa JKT Tanzania na washindi wa pili, Kitayosce ya mkoani Tabora.
Wakati, wageni hao wakifurahia matokeo mazuri,Mbeya City ni Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zimeshuka kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasisitiza kuwa, huu mchezo w asoka ni bora uchezwe kote. Endelea;

1.Ningekuwa ninaweza, timu ningeziongeza,
Kila mkoa mkoa kuweza, Ligi Kuu kuingiza,
Wako vijana waweza, hawatashindwa kucheza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote
2.Imenifanya kuwaza, lile limenitokeza,
Kwa Mashujaa kuweza, Mbeya City garagaza,
Kigoma sasa kuanza, Ligi Kuu kuicheza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
3.Mpira wanapocheza, burudani waongeza,
Na watu wajiongeza, viwalo wanaongeza,
Wanapita wapendeza, sare zinavyopendeza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
4.Vijana wanaocheza, pengine ngewapoteza,
Wangekwenda wakaoza, na maisha kudumaza,
Sasa wanajitangaza, hata pesa waingiza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
5.Haya nayo nayawaza, timu ziweze kucheza,
Viwanja kuviongeza, vile vinajieleza,
Mpira kuusogeza, vizuri waweze cheza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
6.Viwanja vya kupendeza, na walimu wanoweza,
Makosa kuyapunguza, vijana waweze cheza,
Hapo tutatokomeza, vijana mayai viza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
7.Sasa Kigoma wacheza, na Kagera wanacheza,
Tanga nako wanacheza, hata Lindi wanacheza,
Dasalama wanacheza, Morogoro wanacheza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
8.Geita wanauweza, Singida waliucheza,
Mikoa gani ongeza, ligi kuu wanacheza?
Nuru lini taongeza, nao waweze kucheza?
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
9.Mtwara wamejilaza, Ruvuma yajidumaza,
Songwe nenda uliza, kipi kinachowakwaza,
Manyaza wajiongeza, lakini hawajaweza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
10.Tabora wasindikiza, Simiyu nenda uliza,
Iringa wajipongeza, kubeti wajiliwaza,
Katavi lini taweza, Rukwa nao kuongoza?
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
11.Kombe la Taifa waza, mikoa lijisogeza,
Kitaifa kutangaza, vijana wanaoweza,
Hilo walishadumaza, hamasa kuipunguza,
Huu mchezo wa soka, ni bora uchezwe kote.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602