Rais Dkt.Mwinyi ahudhuria ufunguzi wa Olimpiki Maalum Berlin

BERLIN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amehudhuria sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu mwaka 2023 katika uwanja wa Olimpia Jijini Berlin nchini Ujerumani jana tarehe 17 Juni 2023.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki katika michezo hiyo ikitafuta medali kwenye mpira wa wavu na riadha. 

Rais Dkt.Mwinyi katika msafara wake ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Pindi Chana, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dk.Abdallah Saleh Possi.Mashindano hayo yamefunguliwa jana tarehe 17 Juni na kumalizika 25 Juni 2023.

Awali,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mama Mariam Mwinyi walijumuika katika hafla fupi ya chakula cha mchana na wachezaji 20 wa Timu ya Tanzania inayoundwa na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanaoshiriki mashindano ya Olimpiki kwa watu wenye mahitaji maalum. 
Hafla hiyo ya chakula cha mchana ilifanyika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani. Aidha, Rais Dkt.Mwinyi aliwatia moyo na kuwatakia kila heri katika mashindano hayo pamoja na kuwaalika Zanzibar pindi watakapomaliza mashindano. 

Mwaka 2019 Tanzania iliibuka mshindi wa Dunia katika michezo ya Mpira wa Wavu na riadha na kuibuka washindi ambapo timu hizo zilipata medali ya shaba Abu Dhabi, UAE.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news