NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa India anayefanyia kazi zake Zanzibar, Dkt.Kumar Praveen aliyefika Ikulu kujitambulisha.
Mazungumzo yao yamegusia masuala kadhaa muhimu ikiwemo Miradi ya Maji safi na salama Zanzibar, wamejadili Chuo cha Ufundi na Amali Pemba kinachotoa mafunzo ya ufundi na ujuzi kwa vijana.
Aidha, wamezungumzia ufadhili wa masomo kutoka India ikiwa ni fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka Zanzibar kwenda India kusoma katika vyuo au taasisi za elimu ya juu.
Wakati huo huo, Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano na ufadhili wa miradi ya maji ambayo inatekelezwa kupitia mkopo wa Benki ya Exim India.
Vilevile, Balozi Mdogo Dkt.Kumar Praveen amemweleza Rais Dkt.Mwinyi kuhusu ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Dkt.Subrahmanyam Jaishankar anayetarajiwa kuja nchini mwezi Julai mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa Miradi ya Maji Zanzibar.
Ujio wa Waziri Jaishankar unaashiria nia ya India kuendeleza ushirikiano wake wa karibu na Zanzibar.