NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemwapisha Dkt.Said Khamis Juma kuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Said Khamis Juma, baada ya kumaliza kumuapisha, hafla hiyo iliyofanyika Juni 10, 2023 katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said. (Picha na Ikulu).
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Juni 10, 2023 Ikulu jijini Zanzibar kabla ya kuanza kikao cha Tume ya Mipango.
Rais Dkt.Mwinyi ameendelea kuweka msisitizo katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na uwajibikaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengo likiwa ni kuhakikisha ufanisi wa matumizi ya rasilimali za umma.
Dkt.Said Khamis Juma Naibu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali atamsaidia Dkt.Othman Abbas Ali Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanafanyika kwa uwazi, ufanisi, na kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.