Rais Dkt.Mwinyi atembelea Makumbusho ya Fuer Naturkunde jijini Berlin

BERLIN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea Makumbusho ya Fuer Naturkunde jijini Berlin, Ujerumani tarehe 19 Juni 2023 .
Makumbusho haya yamehifadhi mabaki ya Dinosau ( Dinosaur) mkubwa aliyegunduliwa Tanzania Mwaka 1906/07 katika Kijiji cha Tendaguru Lindi.

Masalia hayo yanakadiriwa kuwepo wakati wa Kipindi cha Jurassic cha mwisho takribani miaka milioni 150 iliyopita. 

Pia ametembelea ukuta wa Berlin uliokuwa ukitenganisha Berlin ya Mashariki na Magharibi uliojengwa 13 Agosti 1961, ulidumu hadi 9 Novemba 1989. 

Ukuta huo ulijengwa na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (GDR) kwa lengo la kuzuia raia wa Mashariki ya Ujerumani kutoroka kwenda Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news