Rais Dkt.Mwinyi kushiriki Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuondoka Zanzibar leo Juni 15, 2023 kuelekea Ujerumani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu (Special Olympics World Games).

Ni mashindano ambayo maelfu ya wanamichezo wenye mahitaji maalumu kushindana katika michezo mbalimbali, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 17 hadi 25 Juni 2023.

Kwa upande wa Tanzania, Chama cha Olimpiki Maalumu (Special Olympic) Tanzania kitashirikisha wachezaji 21, makocha pamoja na viongozi wa michezo ya mpira wa wavu na riadha wakisindikizwa na Waziri mwenye dhamana Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, Charles Hilary, Rais Dkt.Mwinyi anatarajiwa katika safari hiyo kuambatana na Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Habari Vijana na Michezo, Mhe.Tabia Mwita pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mbali na kushiriki uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin, Rais Dkt, Mwinyi pia atakutana na viongozi wa juu wa Serikali nchini humo, Wakuu wa Mashirika mbalimbali, Wawekezaji na jamii ya Watanzania waishio Ujerumani (Diaspora).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news