NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Tanazania inatambua na kuheshimu usawa wa kijinsia kwa kuona umuhimu wa kuwachagua wanawake kwenye mihimili yote ya Serikali, Bunge na Mahakama kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ni waliofika kumkabidhi tunzo ya hongera kwa mafaniko makubwa aliyofanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
Alisema, serikali zote mbili zitaendelea kutoa fursa za kutosha kwa wanawake kwenye maeneo mbalimbali ili kutekeleza azma yao kufikia 50 kwa 50.
Alisema maendeleo yana taka kwa usawa wakijinsia kutoa haki na fursa sawa katika maendeelo ikiwemo elimu, afya na jamii kwani kumuelemisha mwanamke kutaondoa changamoto nyingi kwenye jamii
“Sijajuta hata kidogo kwa wale wanawake niliowateua kwenye Serikali yangu, kwa kweli naona umuhimu wa kuwaongeza kwenye safu mbalimbali” Alibainisha Rais Dk. Mwinyi.
Aidha, alisema Serikali pia itaendelea kuimarisha huduma za mama na mtoto ili kupunguza changamoto nyingi kwa wanawake.
Rais Dkt. Mwinyi pia aliwapongeza ULINGO kwa kazi kubwa wanayoifanya kuunganisha pamoja sauti ya pamoja, na kuwasifu hatua yao ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa kwa kuunganisha nguvu ya umoja wao bila kujali tofauti ya itikadi zao za kisiasa pamoja na kuwashirikisha wanawake wengi na kuwashajihisha kitaaluma kujua haki na wajibu wao kwenye masuala haki na siasa.
Alisema, katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki kwa jinsia zote kushiriki katika masuala siasa. Pia Dkt. Mwinyi aliahidi kuipokea tunzo hiyo kama sehemu ya kuongeza za kuweka fursa sawa za jinsia kwenye maeneo yote.

Pia, walimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kutambua kikwazo kimubwa kinachowanyima fursa wananwake ikiwemo ukosefu wa elimu, changamoto kwenye sekta ya afya kwa kuweka miundombinu imara ili kukabiliana na changamoto pamoja na huzitatua kwa kipindi kifupi cha uongozi wake.
Akizungumza kwenye halfa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Anna Magareth Abdalla, Makamu Mwenyekti wa taasisi hiyo kwa Zanzibar ambae pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan alimuahidi Dk. Mwinyi mwaka 2025 atarejeshwa tena madarakani kwa nguvu na umoja wa wanawake nchini ambao kwasasa sauti yao ni moja tu ya kudumisha amani yanchi na maendeleo kwa maslahimapana ya taifa.
Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Dkt.Mwinyi kwa kwa mageuzi makubwa aliyoiletea Zanzibar kupitia sekta za Afya, Elimu na Uchumi wa Buluu pamoja na kuongeza fursa za uongozi na maendeleo kwa wanawake na kumuahidi daima wanamuunga mkono katika kuiletea maendeleo makubwa Zanzibar.