NA DIRAMAKINI
RAIS wa Baraza la Mitume na Manabii Tanzania,Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala ametangaza rasmi kuwa, Julai 7, mwaka huu litafanyika jambo kubwa mjini Morogoro ambalo licha ya kuikumbuka siku yake ya kuzaliwa yatafanyika maombi maalum kwa kila mwenye uhitaji na wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambapo watapokea uponyaji wa papo kwa papo.
Dkt.Nabiijoshua ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania yenye makao yake Yespa Kihonda mjini Morogoro amefafanua kuwa, siku hiyo kila mmoja asikose kufika kwani Mungu atajidhirisha kwa wote.
"Nichukue nafasi hii kuwakaribisha tarehe 7 mwezi wa 7, 2023 wote kwa Nabiijoshua mjini Morogoro kwenye sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Rais wa Baraza la Mitume na Manabii Tanzania ambaye ni mimi ndugu yenu, Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala,"amefafanua Rais Dkt.Nabiijoshua.
Sauti ya Uponyaji Tanzania huwakutanisha maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Morogoro ambapo kila ambaye hupata nafasi ya kufika hapo hupokea uponyaji na hitaji la moyo wake katika jina la Yesu Kristo.