NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua, Prof. Abel N. Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI) akichukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.
Kabla ya uteuzi huo, Prof. Makubi amewahi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali kisha baadaye akawa Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Pia,Rais Samia amemteua Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Dkt.Mohahemed Gharib Bilal, Makamu wa Rais mstaafu ambaye amemaliza muda wake.
Amemteua pia Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Dkt. Mzee alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Y. C. Lumbanga aliyemaliza muda wake.
Mwingine aliyeteuliwa ni Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenvekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Ple kwa kipindi cha pili na uteuzi huu umeanza Juni 6, 2023.