Serikali yaahidi mema zaidi kwa sekta binafsi

NA ELEUTERI MANGI-WUSM 

KATIBU Mkuu Wizara ya UItamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi hatua inayosaidia kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo ya sekta nyingine.
Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Juni 17, 2023 wakati wa Mahafali ya 13 ya Shule za Kimataifa za Feza kwa manufaa ambapo wanafunzi wa shule ya msingi darasa la sita, sekondari darasa la 11 na 13 wamehitimu masomo yao.
“Tunapaswa kutambua vipaji vya watoto na vijana katika michezo na utamaduni, hivyo tulilazimika kuwa na programu zinazojumuisha utendaji wa kitaaluma na kukuza vipaji kwa wanafunzi wetu kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi,” amesema Bw. Yakubu.

Aidha, amewasihi Viongozi na walimu wa Shule za Kimataifa za Feza kuendelea kuthamini na kutekeleza moja ya haki za Mtoto zinazohusiana na Michezo na Utamaduni ambayo inafafanua haki ya Watoto kucheza na kushiriki katika shughuli za michezo na kitamaduni kwa manufaa ya kimwili, kiakili na kiafya. 
Michezo inatoa ajira kwa vijana wengi Tanzania, Afrika na duniani kote na ni moja kati ya shughuli muhimu zinazopaswa kutekelezwa kwa kuzingatia azimio la mkutano wa Umoja wa Vijana wa Utamaduni na Michezo wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2016.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news