Serikali yagharamia usafiri kwa timu ya Olimpiki Maalum

NA SHAMIMU NYAKI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara kupitia Baraza la Michezo Tanzania imegharamia tiketi 15 za ndege zenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa timu ya Olimpiki Maalum inayokwenda kushiriki mashindano ya Dunia katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia Juni 17 hadi 25 mwaka huu. 
Mhe. Chana amesema hayo leo Juni 10, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi Bendera kwa Timu hiyo inayokwenda kushiriki mashindano hayo akiwataja pia Wadau waliounga mkono safari hiyo ambao ni Bodi ya Special Olympic ambayo imetoa tiketi 8 za thamani ya Shilingi Milioni 26. 8 na Azam Media tiketi 2 za Milioni 6.7. 

Wadau wengine ni Sibusiso Foundation Arusha ambao waligharamia Kambi ya Mazoezi Jijini Arusha na ASAS ambao wametoa fulana 50 zenye thamani ya Shilingi Milioni 1.2. Kufuatia michango hiyo, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amewashukuru wadau hao pamoja na kuwakaribisha wadau wengine waendelee kuunga mkono shughuli za michezo hapa nchini. 
"Nawapongeza Viongozi wa Special Olympic Tanzania na Wadau wote ambao wamechangia kufanikisha maandalizi ya safari hii, nawatakia heri vijana wetu, nendeni mkaliwakilishe vyema Taifa letu, tuko nyuma yenu tunawaombea," amesema Mhe. Chana. 

Michezo hiyo hufanyika kila baada ya miaka minne, ambapo mara ya mwisho imefanyika mwaka 2019, Abudhab Flame za Kiarabu, Tanzania ilishiriki katika mchezo wa Mpira wa Wavu na kuibuka mabingwa kwenye mchezo huo pamoja kupata medali ya Fedha kwenye mchezo wa Riadha

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news