NA LUSUNGU HELELA
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema itaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha uadilifu, uwajibikaji na utawala bora katika Utumishi wa Umma ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa maendeleo ya taifa.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji akizungumza Jijini Dodoma na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika na upande wa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Amesema Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama hivyo vya Kitaaluma vina jukumu kubwa la kusimamia dhana ya utawala bora nchini ili kuongeza uwazi na uwajibikaji zaidi katika Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.
Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
"Utawala bora, ni ile dhana inayozingatia maslahi mapana ya taifa, hivyo ninyi Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma muhakikishe huduma mnazozitoa zinazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji, haki sawa, demokrasia na kuwasikiliza watu wengi na wachache," amesisitiza Bw. Ngangaji.
Amefafanua kuwa, utaratibu wa kuwakutanisha Wataalamu hao kutasaidia kutoa mapendekezo ya namna ya kubadilisha na kuboresha Miongozo ya Usimamizi wa Maadili kwenye Taasisi hizo katika kusimamia dhana ya utawala bora nchini.
Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewataka wasimamizi hao wa maadili kuhakikisha wanawachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao wanakiuka maadili huku akisisitiza kuwapongeza na kuwatia moyo watumishi ambao wanafanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji kuzungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi.Leila Mavika amesema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kubaini changamoto za usimamizi wa maadili ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kusimamia maadili kutokana na uzoefu wanaokutana nao.
"Sisi tunaangalia maadili katika masuala ya Utumishi wa Umma lakini kwa wenzetu waliopo kwenye Vyama vya Kitaaluma wanaangalia madili ya kitaaluma kwani wapo Watumishi wa Umma ambao ni wanachama wa vyama hivyo," amesisitiza Bi. Mavika.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa waandamizi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kuzungumza nao kwenye kikao kazi na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji, Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Baraza la Uuguzi na Ukunga, Bi. Jane Mazigo amesema kikao hicho ni muhimu kwao kama wadau muhimu wa usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Utumishi wa Umma katika Vyama vya Kitaaluma hivyo, anaamini kitatoa mwelekeo mpya katika kuhakikisha wanabadilishana uzoefu kutokana na changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.