NA DIRAMAKINI
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameondoka nchini leo tarehe 12 Juni, 2023 kuelekea Marrakesh, nchini Morocco.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Kibunge wa Majadiliano kuhusu Dini mbalimbali (Conference on Interfaith Dialogue) utakaofanyika nchini humo Juni 13 - 15, 2023.
Aidha, katika Mkutano huo ameambatana na Waheshimiwa Wabunge Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Esther Matiko pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa Mwihambi ndc.