NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa M. Khamis amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Hussein Alvandi Behineh, Balozi wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran nchini Tanzania yaliyofanyika katika ofisi za Balozi.

Katika kikao hicho wamejadili kuhusu ushiriki wa Iran kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na siku maalum ya Iran kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Iran ili kubadilishana fursa baina yao.
