NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa Khamis amepokea udhamini wa viti, meza na vizimba 170 vya mabanda ya maonesho vyenye thamani ya shilingi milioni 300.
Ni kutoka kwa kampuni ya manunuzi ya East Africa Commercial and Logistic Center ambao pia ni wadhamini wakuu wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo Juni 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi.Latifa Khamis amesema, TanTrade imewaza kuokoa fedha zaidi ya shilingi milioni 100 zilizokuwa zinatumika kukodisha vifaa hivyo ili kukidhi mahitaji ya washiriki katika maonesho hayo.
Naye Meneja Mkuu wa East Africa Commercial and Logistic Center (EACLC), Bi.Wang Xiangyu amesema, wana furaha kuwa wadhamini Wakuu wa Maonesho ya 47 ya DITF, 2023 na hiyo ni hatua ya mwanzo wa ushirikiano kati ya TanTrade na kampuni hiyo na amewakaribisha watembeleaji kutembelea banda kubwa la nchi ya China (China Pavellion) linaloratibiwa na kampuni hiyo lililopo kwenye Maonesho ya SabaSaba.
Ni banda lenye ushiriki wa makampuni zaidi ya 50 ya sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tehema, Mashine na Viwanda, Miundombinu kutoka nchini China