NA LWAGA MWAMBANDE
1. Ukisema Tanzania,
Zanzibar inaingia,
Nchi inayovutia,
Atanipeleka nani?
2. Ubora nakutajia,
Unguja ukiingia,
Kisiwa kimetulia,
Ndicho kikubwa nchini.
3.Watu wake nakwambia,
Wapole sijasikia,
Napokuzungumzia,
Utafurahi moyoni.
4. Mambo ya kukuibia,
Mageni kwao sikia,
Ni sisi wa kufikia,
Mechafua visiwani.
5.Wenyewe wametulia,
Yao wanajifanyia,
Kama ukiwafikia,
Uungwana tabaini.
6.Huku nitakurudia,
Nizidi kukusifia,
Bila wao Tanzania,
Itapotea ramani.
7. Pemba nako kisikia,
Watu wameshatulia,
Maisha wayajulia,
Hawana shaka moyoni.
8.Uzuri wa Tanzania,
Zanzibari twaanzia,
Kilimanjaro jazia,
Na Ngorongoro kundini.
9.Marashi ukisikia,
Karafuu yachangia,
Nyingi wanajilimia,
Visiwa vinashaini.
10. Mpunga wajilimia,
Na sukari wachangia,
Viwanda ukisikia,
Zanzibar vipo amini.
11. Hili ninakutajia,
Ni kubwa nikikwambia,
Lile linalochangia,
Uchumi wa visiwani.
12. Utalii kisikia,
Ni dhahabu Tanzania,
Ukitaka furahia,
Tembelea visiwani.
13.Hoteli nakuambia,
Hao nawaaminia,
Zingine zinaishia,
Ndani ndani baharini.
14. Moja ninakutajia,
Mjini ukiingia,
Ni Verde ninakwambia,
Tadhani uko mtoni.
15.Na Mji Mkongwe pia,
Kwa kweli unavutia,
Mitaa ukipitia,
Ni fahari ya machoni.
16.Kama Bara Tanzania,
Mikoa inachangia,
Zanzibar mitano pia,
Yaleta uchumi ndani.
17. Kule Pemba Tanzania,
Mikoa miwili pia,
Hiyo tunaisifia,
Ni maarufu nchini.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602
HISTORIA inaonesha kuwa, Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Aidha,kwa ujumla visiwa hivyo vipo baina ya Latitude na Digrii 6 Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudi 39.55 na Digrii 40 Mashariki, Zainzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zanzibar ina miongawanyiko minne ya majira ya hali ya hewa katika mwaka wa Kalenda inayoanzia mwezi Januari hadi Disemba ambayo inahusisha majira ya Kaskazi (Disemba hadi Febuari), Masika (Machi hadi Mei), Kipupwe (Juni hadi Septemba) na Vuli (Oktoba hadi Novemba).
Zanzibar ina jumla ya mikoa mitano, kati ya hiyo, mikoa mitatu ipo katika Kisiwa cha Unguja ambayo ni Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja na mikoa miwili ipo katika Kisiwa cha Pemba ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mkoa wa Kusini Pemba.
Katika kuwasogezea wananchi huduma za kiutawala katika maeneo yao, jumla ya wilaya 11 zilianzishwa ambazo ni Wilaya ya Mjini, Wilaya ya Magharibi A, Wilaya ya Magharibi B, Wilaya ya Kusini, Wilaya ya Kati, Wilaya ya Kaskazini A, Wilaya ya Kaskazini B, Wilaya ya Chake Chake, Wilaya ya Mkoani, Wilaya ya Wete na Wilaya ya Micheweni, ambapo jumla ya Shehia 388 zimeanzishwa ndani ya wilaya hizo. Zanzibar ina eneo la maili 637 za mraba.
Zanzibar ina mchanganyiko wa tamaduni tofauti ambazo zinatokana na wenyeji ambao walikaa pamoja kwa muda mrefu na kuanzisha tamaduni zinazohusisha lugha, dini, mavazi, mapishi, sherehe za mila na za kijadi.
Hata hivyo, asili za tamaduni hizo zilichanganyika na tamaduni za wahamiaji kutoka Asia, Ulaya na Amerika na Visiwa vya Bahari ya Hindi.
Kiswahili ni lugha ya mawasiliano inayotumiwa katika mawasiliano rasmi na kawaida katika jamii mara tu baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964, Serikali ya Zanzibar ilikipa hadhi Kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa itakayotumika katika shughuli zote rasmi za kiutawala na kijamii.
Pia, Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 inatoa mamlaka kwa Benki Kuu pekee kutengeneza na kutoa fedha (Noti na Sarafu) kwa matumizi nchini Tanzania.
Hiyo ndio fedha halali kwa ajili ya malipo nchi Tanzania. Hivyo, Benki Kuu inawajibu wa kubuni na kuagiza noti na sarafu ili kukidhi mahitaji ya fedha nchini na fedha ya Tanzania ni shilingi. Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasisitiza kuwa, ukifanya uamuzi wa kwenda Zanzibar kikazi au kutalii, kamwe hautajutia uamuzi wako. Endelea;